Friday, 15 November 2013

Huyu ndiye Mganga anayedaiwa kutumiwa na Penny, Diamond na Mastaa wengine kujipatia mafanikio yao....! Mganga afunguka kila kitu.... !!

Dk Kamdege
"Mimi hao vijana nawafahamu sana lakini mimi ni Dk wa Watanzania wote sio Pennie na Diamond tu hapana, kazi zangu ainakubadirika na Watanzania wote na hata nje ya nchi kwani mimi nawatolea watu mikosi wanaotaka kuwa maarufu na wenye mafanikio pia nawanyooshea njia kwa hiyo naomba msiseme mimi ni Dk wa Pennie na Diamond hata viongozi wakubwa Serikalini nawapatia baraka zangu kisha wanaenda kufanikiwa. Huwa sipendi kujitangaza huko kwani mimi situmii uchawi kumpa mtu mafanikio, hapana. Hapa ni miti shamba tu inafanya kazi yake."
Alisema Dk Kamdege alivyohojiwa na 'GumzoLaJiji blog.

Diamond na Penny wadaiwa kumtumia mganga huyu ili kupata mafanikio yao...
Mganga huyo wa kienyeji ambae amekuwa maarufu sana tangu aanze huduma kutokana na watu maarufu wengi kumfuata kwa ajili ya kutatuliwa mambo yao ikiwemo mafanikio kwenye biashara, kazi, musiki, sanaa, uongozi wa ngazi za juu pamoja na michezo.

Habari zaidi zilisema miezi kadhaa iliyopita, mganga huyo aliwahi kujitoa kwenye vyombo nya habari akimsihi Pennie aende kwake akamtafutie dawa ili Diamond atulie kwani anamfahamu vizuri mwanamuziki huyo na anajua kitu ambacho angefanya.


Kila siku nikiamka, kuna jipya linaloendelea bongo! Inasikitisha sana. Sasa jinsi hii stori ilivyo, inamaana huyo Penny na Diamond hawakumpa huyo mganga namba zao za simu mpaka mganga aende kumtafuta Penny kwenye nyombo vya habari? Hahahaaaaaa!!! Inabidi nicheke!!
Au ndio kama wanavyosema kuwa kuna watu wanapenda kutumia majina ya watu wanaofahamika ili na wao wajulikane? Haieleweki?! 
Uongo mtupuuuu!!
Mungu wasaidie watu waache ushirikina duuuu!! 



Source: gumzolajiji
Follow me on Twitter @leilamaingu or Facebook @leilamaingu for news, fashion, entertainment, celeb gossip and more....



No comments:

Post a Comment