Monday, 16 July 2012

Baba Mzazi wa Diamond Platnumz alalamika kuwa Diamond hamthamini tangu apate mafanikio...!!



Nasibu Abdul Juma ‘Diamond Platnum’

Mzee Abdul Juma.

Baba yake Diamond(Mzee Abdul Juma) amelalamika kuwa tangu mwanae (Nasibu Abdul Juma 'Diamond Platnumz') hamthamini tangu apate mafanikio. Wale waliodai kuwa ni ndugu za Diamond, waishawahi kusema kuwa Baba wa Diamond (Mzee Abdul Juma) alishafariki dunia tangu 2004.

Aisee hii kali!!


Habari kwa hisani ya Global Publishers

3 comments:

  1. Wapendwa, huyu mzee mimi namshauri aachane na lawama zisizokuwa na mpango. Mlimmwaga Diamond akiwa mtoto, yeye na mama yake wakaishi maisha ya taabu sana. Hakutokea, hakuwakumbuka, hakuchangia. Sasa iweje leo anataka Diamond amhudumie. Yaani mimi hawa wazee design hii wananiboa sana na wapo wengi. Mimi nadhani ni vyema sote tukichukua hali hii kuwa funzo kwa wanaume na wanawake wanaoshit watoto wao. Mtoto hawezi kukuzoea ukubwani kama ulimmwaga utotoni. Nasema haya kwa uhakika kabisa. Nazifahamu vyema hisia za Diamond kwakuwa na mimi baba yangu alinifanyia hivyo hivyo. Alipoona nimemaliza vyuo, nina shahada ya pili, nina kazi nzuri, mama nimemjengea nimemweka pazuri, na yeye akaanza kudai matunzo, tena kwa ukali na kumtishia mama eti atanilaani nifilisike. Jamani, watelekezaji, ACHENI HIZO

    ReplyDelete
  2. Baba Diamond, unavuna ulichopanda, utavuna ulichopanda, ulichopanda, unavunaaaaa! Ulimwengu bwana, ndio mchungaji wako, unavuna ulichopaaandaaaaa! Ulimpanda yeye ukamkataaa, sasa iweje unaona anafaaa? Kosa lake kosa laake, nini baaba, ulimwacha na mama Tandale, bibi akamlea peke yake, kasaidiwa na mamaae na majirani wengi pale, mjomba mkubwa kwa machaale wakati wewe uko mbaaale, sasa hivi inakuwaaje, unataka kula penshene....... Ntakutengenezea jingo baba Diamond, kisha nitaiuza CD kama singo halafu nitakutumia pesa ujihudumie. Achana kabisa na Diamonde

    ReplyDelete
  3. Mzee Abdul: Huko ulikokuwaga miaka yote hakunaga mfwenge, unakaga kulaga wa Nasib sasa? Hakunaga mbaaaaya kama wewe!

    ReplyDelete