Tuesday, 16 July 2013

Bongo Gossip: SAKATA LA SHEIKH ALIYEMWAGIWA TINDIKALI JIJINI ARUSHA SIRI NZITO ZAFICHUKA...!!

Matukio ya kigaidi yanayoendelea kuuandama mkoa wa Arusha, ambapo Shehe Mkuu wa Wilaya ya Mkoa wa Arumeru, Said Juma Makamba amejeruhiwa vibaya kwa kumwagiwa maji yanayosadikiwa kuwa ni tindikali....


Shehe Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Said Juma Makamba.
Tindikali hiyo inadaiwa alimwagiwa na watu
wasiojulikana usiku akiwa nyumbani kwake ambapo kiongozi wa Baraza la Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) mkoani hapa ameanika siri nzito kwa kusema kuwa aliyefanya unyama huo ni gaidi.
 Kaimu Mwenyekiti, Shehe wa Bakwata Mkoa wa Arusha, Abdallah Masoud alisema juzi kuwa Makamba amefanyiwa kitendo cha kigaidi
 ambacho kiliwahi kufanywa pia kwa Katibu wa Bakwata mkoani hapa,
Abdullazizi Jonjo, Oktoba mwaka jana ambapo alilipuliwa na bomu la mkono nyumbani kwake akiwa wamelala na hadi sasa hali yake bado haijaimarika.
Alisema kuwa matukio hayo yamekuwa yakijirudia baada ya jeshi la
polisi kushindwa kuwatia mbaroni wahusika.
Alisisitiza kuwa wanaowafanyia viongozi wa kidini unyama huo wa kigaidi wapo ndani ya Uislamu na wamekuwa wakifanya hivyo kwa lengo la kudhoofisha uongozi wa misikiti.



Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, ACP Liberatus Sabas.
Tumekuwa tukitoa taarifa polisi na kuwataja watuhumiwa lakini hatupati matunda ya kukamatwa kwa wahusika ingawaje wanajulikana,” alidai Shehe Masoud.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, ACP Liberatus Sabas alipoulizwa juu ya tukio hilo alisema kuwa polisi wameanza uchunguzi na alipobanwa kuhusu madai ya ugaidi akaongeza: “Taarifa nitazitoa pindi washukiwa watakapotiwa mbaroni kwani uchunguzi bado
unaendelea na hakuna anayeshikiliwa hadi sasa.”
Gazeti hili lilimtafuta Shehe Makamba aliyelazwa wodi ya majeruhi katika Hospitali
ya Mkoa Mount Meru, anakopatiwa matibabu baada ya kujeruhiwa vibaya usoni, machoni, kifuani na mgongoni akasema kuwa tukio hilo lilitokea saa 5 usiku wa kuamkia Jumamosi iliyopita nyumbani
kwake Morombo jijini hapa wakati wakijiandaa kulala.
Shehe huyo ambaye pia ni Imamu wa Msikiti wa Sekei wilayani Arumeru, alieleza kuwa baada ya swala alirejea nyumbani kwake na kabla ya kulala alienda kujisaidia katika choo cha nje na kwamba wakati akirudi ili aingie ndani ghafla aliona mtu akiwa amesimama.
Wakati nikijiuliza kuwa huyu ni nani ghafla mtu huyo alinimwagia majimaji yaliyonilowanisha usoni na kifuani na kuanza kusikia maumivu makali sana sehemu hizo, nikaanza kupiga kelele kuomba msaada kwa majirani ambao walifika na kunileta hospitali kwani macho yalikuwa hayaoni” alisema Shehe  Makamba.
Alidai kuwa anaamini tukio hilo la kigaidi limetokana na ugomvi wa
madaraka ndani ya dini hiyo ambapo kwa muda mrefu kumekuwa na
msuguano wa Waislamu kugombea kuongoza misikiti mbalimbali.





Source: Gumzo la Jiji
Follow me on Twitter @leilamaingu or Facebook @leilamaingu for news, fashion, entertainment, celeb gossip and more.....

No comments:

Post a Comment