Thursday 29 May 2014

Bongo Gossip: Sijavuruga Ndoa ya Vicky Kamata


Suala la kukwama kufungwa ndoa ya Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Vicky Kamata limechukua sura mpya baada ya mzazi mwenza wa mchumba wa mbunge huyo kukanusha taarifa kwamba alikwenda Dodoma kwa lengo la kuomba msaada kwa viongozi wa Bunge.
Kauli ya Mama huyo imezidisha utata katika sakata la kukwama kufungwa kwa ndoa hiyo iliyokuwa ifanyike Jumamosi baada ya kutokea habari kuwa mwanamke  mmoja alikwenda bungeni mjini Dodoma kutaka kuonana na Spika kwa lengo la kuomba Bunge limsaidie kupata haki yake kabla ya harusi hiyo kufungwa na hivyo kusababisha harusi kutofanyika.
Kamata, ambaye alijizolea umaarufu kutokana na wimbo wake wa "Wanawake na Maendeleo" na baadaye kuingia bungeni katika uchaguzi wa mwaka 2010, alikuwa afunge ndoa na mtu aitwaye Charles Gardiner Jumamosi iliyopita jijini Dar es Salaam, lakini haikufayika kutokana na mbunge huyo kuwa mgonjwa kiasi cha kulazwa hospitalini maeneo ya Tabata.
Mzazi mwenza Charles Gardiner, Kinavi Dadi alikanusha kufunga safari hadi Dodoma kwa lengo hilo.  

Alisema, "Ni kweli kwamba Charles ni Baba watoto wangu, lakini sijawahi kwenda Dodoma na wala sifahamu chochote kuhusu safari hiyo. Nadhani inatosha." 
Baadae kidogo, mmoja wa ndugu wa Kinavi, ambae aliomba asitajwe jina lake gazetini, alikiri ndugu yao kufunga ndoa na Gardiner Juni 2004 na kujaliwa kupata watoto wawili lakini walitofautiana na baadaye ndoa yao kuvunjwa mwaka 2012,


Watanzania wenzangu wanapenda sana gossip (udaku). Kama huyo mzazi mwenzake na huyo aliyekuwa bwana harusi mtarajiwa (Charles Gardiner) alikuwa hana tena mahusiano na mama watoto, kwanini ndoa ya Vicky Kamata imekuwa na matatizo? Inabidi huyo Charles na Vicky wote wafanyiwe mahojiano ili kujua ukweli uko wapi badala ya watu kusema vitu ambavyo havikutokea.


Follow me on Facebook @leilamaingu or Twitter @leilamaingu for news, fashion, entertainment, celeb gossip and more....



No comments:

Post a Comment