Friday 6 September 2013

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdukrahaman Kinana Septemba 10 anatarajiwa kuanza ziara ya kawaida katika mikoa ya shinyanga, Simiyu na Mara.

Ziara hiyo itaanzia katika mkoa wa Shinyanga Septemba 10 mpaka 13 mwaka huu, kwa kutembelea wilaya zote nne za mkoa huo na kufuatiwa na mkoa mpya wa Simiyu kuanzia Septemba 14 mpaka Sptemba 19 kwa kutembelea wilaya zote tano kabla ya kuhtimisha ziara hiyo kwa kutembelea wilaya Sita za mkoa wa Mara kuanzia Septemba 20 mpaka 25 mwaka huu.

Katika ziara hiyi, Katibu Mkuu wa CCM attambatana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM anayeshughulikia itikadi na Uenezu Ndugu Nape Nnauye.

Kwa mujibu wa Ratiba ya ziara hiyo, Wajumbe hao wa sekretarieti watakagua uhai wa Chama ikiwa ni pamoja na kupokea wanachama wapya sanjari na kuhamasisha wananchi kujituma katika shughuli za uzalishaji ili kuleta tija katika maisha yao na ya Taifa kwa ujumla.

Aidha watakagua maendeleo ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010/2015 hasa katika miradi ya kimaendeleo kama vile Ujenzi wa majosho kwa ajili ya wafugaji, maendeleo ya maboresho ya kilimo cha Pamba, Uvuvi wenye tija pamoja na maboresho ya sekta za Afya, elimu na miundombinu zikiwemo Barabara.

Katika ziara hiyo, Katibu Mkuu atapata fursa ya kusikiliza kero mbalimbali za wananchi kwa kushauriana na serikali kutafuta nama ya kuzitafutia ufumbuzi. Katibu Mkuu pia atafanya mikutano ya ndani na ya hadhara katika kila wilaya za mikoa hiyo.


By: Nape Moses Nnauye
Katibu wa Itikadi na Uenezi 
05/09/13
Credit: JestinaGeorgeMeru/Twitter
Follow me on Facebook for news, Fashion, entertainment, celeb gossip and more......


No comments:

Post a Comment