Showing posts with label Serengeti Fiesta 2012 Tabora. Show all posts
Showing posts with label Serengeti Fiesta 2012 Tabora. Show all posts

Saturday, 8 September 2012

Tabora Serengeti Fiesta 2012...


Mmoja wa wasanii mahiri katika miondoko ya hip hop hapa nchini,Mwana FA akiwaimbisha wakazi wa mji wa Tabora wimbo wake wa Yalaiti,usiku wa kuamkia leo katika viwanja vya Ally Hassan Mwinyi,ambapo wakazi wa mji huo walijitokeza kwa wingi.Tamasha hilo jumapili litakuwa linarindima mjini Singida katika kiota cha marahaa kiitwacho Singida Motel.
 
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Mabeste akikamua kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012 usiku wa kuamkia leo kwenye uwanja wa Ally Hassan Mwinyi,ambapo katika tamasha hilo wakazi wa mji wa Tabora walijitokeza kwa wingi na kujishuhudia vipaji mbalimbali vya muziki.