Majangaaa! Mwenyekiti wa Klabu ya Bongo Movie, Steven Nyerere na muigizaji Adam Haji 'Baba Haji' nusura wazichape baada ya kupishana kauli kwenye msiba.
Mwenyekiti wa Bongo Movie 'Steve Nyerere' (aliyeshika chupa ya maji) akilia kwa uchungu katika msiba wa Recho.
Uwanja wa vita ulikuwa kwenye msiba wa mwigizaji mwenzao Sheila Haule 'Recho', Sinza-Palestina, jijini Dar ambapo chanzo kilishuhudia mtiti huo, kilidai tatizo liliibuka mara baada ya Steve Nyerere kumchimba mkwara Baba Haji asijiweke karibu na Jacob Steven 'JB'.
"Hata haikujulikana kw anini Steve hakutaka Baba Haji awe karibu na JB, akammaindi ndipo mtiti ulipoibuka, wakataka kushikana mashati bahati nzuri Mtitu (Wiliam) akawaamulia," kilielezwa chanzo.
Akizungumzia sakata hilo baado ya kutulizwa 'munkari', Baba Haji alisema anamshangaa Steve kwa kumchimba mkwara asikae na JB pasipo kuwa na sababu za msingi.
Muigizaji mkongwe wa Bongo Movie, Adam Haji 'Baba Haji' (kushoto) akishiriki kubeba jeneza lenye mwili wa marehemu Recho.
Credit:globalpublishers/tuangazebongoblog
Follow me on Facebook @leilamaingu or Twitter @leilamaingu for news, fashion, entertainment, celeb gossip and more....