Friday, 25 October 2013

Uswisi sasa kurejesha mabilioni ya mafisadi....

"Tanzania haijafanya maombi rasmi hapa Uswisi na hivyo wao kama benki hawawezi tu kutoa taarifa bila kuombwa. Sheria yao imerekebishwa ambapo sasa ni wajibu wa mwnyw akaunti kusema kama fedha zake ni halali au hapana."

Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (katikati) akiwa na maafisa wa Serikali ya Uswiss pamoja na timu ya uchunguzi kufuatilia mabilioni ya fedha zilizowekwa katka benki za nchi hiyo. Picha na Bernard Reinhold.

Dar es salaam, Sakata la vigogo kuficha mabilioni ya shilingi katika benki za Uswisi, limechukua sura mpya baada ya Serikali ya nchi hiyo kutunga sheria inayowabana walioweka fedha kwenye benki za kuzithibitisha, la sivyo zitarejeshwa katika nchi husika.

Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe alifanya mazungumzo na Serikali ya nchi hiyo ambayo imemweleza kuwa imebadili sheria zake ili kuwadhibiti wageni wanaoficha fedha nchini humo.


Kwa habari zaidi, bofya hapa....

Source: www.mwananchi.co.tz
Follow me on Twitter @leilamaingu or Facebook @leilamaingu for news, fashion, entertainment, celeb gossip and more....

No comments:

Post a Comment