Endless Fame Producer Rashid Mohammed 'Chid Classic'
Managing Director of Endless Fame Wema Issac Sepetu
Baada ya kudaiwa kufanya ngono katika magari ya Kampuni ya Endless Fame inayoongozwa na Wema Issac Sepetu, Producer Rashid Mohammed 'Chid Classic' amefunguka na kusema chanzo cha yote ni mshahara na ukuwadi ndani ya kampuni hiyo wala siyo uzinzi. Akizungumza na mwandishi wa gazeti la Gumzo la Jiji, Chid amesema hajafukuzwa katika kampuni hiyo kama alivyodai mratibu wa kampuni hiyo, Petit Man bali ameondoka baada ya kuchoka kufanya kazi bila ya kulipwa mshahara.
Rashid aliendelea kuongea na kusema, " Ni uongo kusema kwamba nimenaswa nikifanya uzinzi Coco Beach nikiwa ndani ya magari ya Wema. Sijawahi hata siku moja kufanya hivyo kwani nina kwangu ambako nina uwezo wa kumwingiza mwanamke wakati wowote.
Tangu kampuni ianzishwe haijawahi kulipa mishahara, unadhani nitakuwa na moyo wa kufanya kazi, sikwenda pale kufanya ukuwadi kama wengine, tena nawaomba wasiendeleekusema uongo kwani nina mengi nayajua ya Endless Fame."
Watanzania wengine wanamatatizo sana! Wakiona mtu anamaendeleo tu basi, watajaribu kufanya kila kitu ili tu wamharibie na kumchafulia jina huyo mtu. Hii stori inaonekana sio ya ukweli. Siku zote hizo hao wafanya kazi wengine wa Endless Fame mbona hawajalalamika kuwa hawalipwi mishahara yao?
Ukweli wa hili jambo anayeujua ni Wema Sepetu na huyo mfanyakazi wake 'Chid Classic'
Source:GumzoLaJiji
Follow me on Twitter @leilamaingu or Facebook @leilamaingu for news, fashion, entertainment, celeb gossip and more....