Siku ya jumanne tarehe 16.10.12 Mh Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Kayanza Peter Pinda alipata fursa ya pekee ya kukutana na baadhi ya watanzania waishio nchini Uingereza katika ofisi za Ubalozi wetu zilizopo hapa jijini London ili kuongea, kufahamiana nao na kuwapa taarifa kamili kuhusu hali ya nchi Kiuchumi, Kisiasa, Kiusalama, Kimaendeleo na changamoto mbalimbali zinazozikabili taifa letu.
Mh Waziri Mkuu alieambatana na mkewe mama Tunu Pinda walipokelewa rasmi na Mh Balozi wetu Peter Kallaghe, wafanyakazi pamoja na maofisa kutoka ngazi mbalimbali katika Ubalozi wetu. Kabla ya kuanza hotuba yake Mh Balozi alichukua fursa hii kuwakaribisha na kuwashukuru watanzania wote ambao waliojitokeza kuja kumsikiliza na kumsalimia Mh Waziri Mkuu.
Akihutubia watanzania zaidi ya mia tatu Mh Waziri alianza kwa kuongelea hali halisi ya uchumi nyumbani ambayo inaendelea kukua vizuri taratibu siku hadi siku tokea Mh Raisi Jakaya Mrisho Kikwete aingie madarakani mnamo mwaka 2005. Kutokana na twakwimu za hivi kutoka idara ya uchumi zinaonyesha kukua kwa GDP kutoka asilimia 6.9% mpaka 7% kwa sasa ambayo imesababishwa na upanukaji kiuchumi. Vile vile pato la wastani kwa mtanzania wa kawaida linazidi nalo kuongezeka taratibu japokua sio kwa kasi kubwa kama ambavyo ingetakiwa. Kwa sasa Mtanzania wa hali ya chini anaishi chini ya dolla moja ($1.00) kwa siku.
Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 imedhamiria kuwa Tanzania iweze kunyanyuka na kuingia katika ngazi ya Kati au Middle Income Country ifikapo mnamo mwaka 2025.
Mwaka 2011-2012 changamoto kubwa ambayo imekua ikikabili Taifa letu ni mfumuko wa bei za vyakula hususani mahindi, Mchele, sukari ambayo imetokana na uuzwaji wa vyakula kwa nchi jirani kama Kenya, Somali, na Sudani ya kusini kwa bei ya ghali na kufanya gharama kuongezeka nchini. Pia kumekuwepo kwa njaa nchini katika wilaya ya kaskazini, kanda ya ziwa na Shinyanga ingawaje hatua madhubuti zimeshachukuliwa ili kuhakikisha tunajitosheleza kwa chakula na zaidi ya hapo kuwekuwepo na mikakati mizuri itaiwezesha Tanzania kuwa ''Bread Basket kwa East Africa'' kwa kulisha sehemu nchi zingine katika jumuiya ya Afrika Mashariki
Tatizo la umeme ambalo bado limekua sugu linasababishwa na kupanda kwa gharama za mafuta ya uendeshwaji.
Mapato ya ndani yanazidi nayo kuongezeka mfano TRA mwaka 2000 walikua wanakusanya bilion 64 kwa mwezi wakati sasa hivi makusanyo ni kiasi cha sh bilion 650 kwa mwezi japokua mahitaji ya nchi ni makubwa mno kuliko mapato yanayokusanywa. Pia mauzo ya nje nayo yanazidi ya zamani.
Uwekezaji wa ndani ya nchi ni Doller 900 ($900 ml)
Ili kukabiliana na hizo Changamoto zinazozidi kukua siku hadi siku Tanzania imejipanga vizuri ili kuimarisha uchumi na maendelo kwa ujumla. Mh Raisi Kikwete amerejesha timu ya mipango inayosimamiwa Dr Mipango ambaye ndio mtendaji mkuu ili kuhakisha mipango yote inayopendekezwa ifanyike kama ilivyopangwa. Tanzania imeweka mipango ya muda mrefu ambayo ni miaka kumi na tano (15) ijayo. Miaka hiyo nayo imegawanywa katika kipindi cha miaka mitano mitano ili kutekeleza azma yake kwa ufanisi zaidi. Mh Waziri Mkuu aliendelea kufafanua kuwa Agenda kuu ya miaka hii mitano ya kwanza Tanzania vipaumbele vimewekwa katika sekta zifuatazo:
a) Ujenzi na upanuzi wa Miundo Mbinu kama Barabara, Reli, Bandari, Viwanja vya ndege, Nishati na mkondo wa Taifa
b) Kilimo- Kuongeza zana za kilimo bora kama matrekta, Mbolea, mbegu bora na kuwawezesha wakulima wadogo wadogo kutumia teknolojia mpya ya kilimo pamoja na kilimo cha umwagiliaji.
c) Kuwekeza na kujenga Viwanda ( Processin Industry)
d) Maji safi na Taka
e) Rasilimali watu
Serikali ya Tanzania imedhamiria kuongeza megawati wa umeme toka zilizopo sasa hivi ambazo ni megawati 600 mpaka megawati 2780 ndani ya miaka ijayo ili kuweza kukomesha tatizo la mgao wa umeme ambalo lina gharimu taifa letu fedha nyingi na kurudisha maendeleo nyuma. Bandari ya Dar inapanuliwa pia ujenzi wa bandari mpya ya Bagamoyo umeshakamilika pesa na mkandarasi vimeshapatikani imebakia kuanza kazi.
Tanzania kuwekua na wimbi kubwa la uwekezaji ambapo nchi nyingi za magharibi zinakimbilia kuja kuwekeza nchini kwetu hasa baada ya kugundulika kwa gesi, makaa ya mawe, dhahabu na Uranium nyingi.
Katika kuhitimisha hotuba yake Mh Waziri Mkuu aliongelea hali ya kisiasa nyumbani na usalama. Kwa ujumla Tanzania bado ni kisiwa cha amani na utulivu kulinganisha na sehemu zingine ingawaje alizungumzia matukio mbalimbali ya hivi karibuni ya vurugu kama ya kuchoma makanisa mbagala, na visiwani Zanzibar, mauaji ya raia wakati wa maandamo Morogoro, Arusha na ya mwandishi wa habari David Mwangosi alieuwawa na polisi pamoja na mauaji ya kutisha ya RPC Barlow Mwanza. Mh Waziri Pinda aliwaomba na kuwasihi watanzania wote kuendelea kufuata sheria pia kuwa watulivu manake mambo yote yamefikishwa mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake. Pia aliwaushuri watanzania wasiogope kurudi nyumbani mara wamalizapo masomo au kuwekeza zaidi nyumbani ili kuweza kujenga taifa letu
Mwishoni kulikuwa na kipindi kirefu cha maswali na majibu ambapo watanzania mbalimbali walipata fursa ya kumwuliza Mh Waziri Mkuu maswali na kutoa maoni au mapendekezo yao kuhusu kero na madukuduku.
MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU WABARIKI WATANZANIA
Asanteni
Urban Pulse Creative wakishirikiana na Miss Jestina Blog
Dr Hamza akisema machache
Mh Balozi Peter Kallaghe akinkaribisha Mama Tunu Pinda kabla Mh Waziri Mkuu kuongea na watanzania
Mh Waziri Mkuu akifafanua jambo
Mh Waziri Mkuu akisalimiana na baadhi ya Watanzania baada ya mkutano
Mh Waziri Mkuu akisoma kitabu cha wageni kabla ya kuweka sahihi
Mh Waziri Mkuu aliongozana na mkewe akisalimiana na Balozi Peter Kallaghe mara baada ya kuwasili Ubalozini
Mh Waziri Mkuu Mizengo Pinda akizungumza na Watanzania
Wakati wa maswali na majibu
Watanzania wakifuatilia hotuba ya Mh Waziri Mkuu
Watanzania wakimsikiliza Mh Waziri Mkuu
Source: Jestina George
Follow me on Twitter @leilamaingu or Facebook @leilamaingu for news, fashion, entertainment, celeb gossip and more....